Thursday, May 21, 2015


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Rama amekuwa na mchango mkubwa katika kukinusuru kikosi cha Coastal Union kuporomoka daraja msimu huu.'

MABINGWA wa Kenya, Gor Mahia wamejipanga kumsajili kwa mara nyingine kiungo mshambuliaji wa Coastal Union, Rama Salim wakati wa usajili wa Juni mwaka huu.

Rama amekuwa akiwatumikia mabingwa wa Tanzania Bara 1988, Coastal Union aliojiunga nao Juni 2014 akitokea Gor Mahia, na mkataba wake wa mwaka mmoja utamalizika mwezi ujao na anahusishwa kutaka kurejea katika Ligi Kuu ya Kenya (KPL).

Naibu Katibu Mkuu wa Gor Mahia, Ronald Ngala, amekaririwa na moja ya mitandao ya michezo ya Kenya leo akieleza kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Congo United ameonyesha nia ya kurejea klabuni hapo na tayari wameshaanza mazungumzo naye ili arejee kwa mara ya tatu.

"Ameonesha nia ya kurejea katika klabu yetu na tumeshaanza mazungumzo naye kuona kama tunaweza kumuingiza katika orodha ya nyota wetu. Ni mchezaji mzuri, tunaujua umuhimu wake, lakini tunahitaji kumshirikisha kocha kwanza kuona kama kuna nafasi ya mchezaji huyo katika kikosi chetu kabla ya kumaliza usajili," amesema.

Rama alijiunga na Gor kwa mara ya kwanza Januari 2012 akitokea Congo United iliyoporomoka daraja, akawaacha mabingwa hao wa Kenya Juni 2013 akitimkia Asia kabla ya kurejea Gor Januari 2014 kwa mkopo wa miezi sita na baada ya mkataba huo kumalizika, akatimkia Tanzania kujiunga na Coastal.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video