Sterling mbioni kuondoka Anfield
LIVERPOOL wanatarajia kufanya mazungumzo na nyota wao kinda Raheem Sterling juma hili baada ya mshambuliaji huyo kumwambia kocha Brendan Rodgers anataka kuondoka Anfield.
Sterling alifanya mazungumzo binafsi na Rodgers kabla ya sare ya 1-1 waliyopata dhidi Chelsea siku za karibuni na aliweka wazi kuwa hataki kuendelea kukaa Anfield.
Lakini nyota huyo wa kimataifa wa England amekubali kufanya mazungumzo ya mwisho na klabu hiyo wakati huu majogoo wa jiji wakikazana kumshawishi aendelee kukaa Merseyside.
Sterling amegoma kusaini mkataba mpya wa miaka mitano na klabu yake kwasababu haridhishwi na uwezo wa klabu hiyo kushindania ubingwa.
Mshambuliaji huyo anataka kuendelea kucheza ligi ya mabingwa ulaya, kitu ambacho kitakosekana Anfield msimu ujao.
Pia anaona kama hathaminiwi kwa kuambiwa atalipwa paundi elfu 90 kwa wiki katika mkataba mpya uliopo mezani kwasasa.
0 comments:
Post a Comment