Monday, May 18, 2015

Michel Platini amesema haamini kama kiungo wa Juventus Paul Pogba yuko katika kiwango sawa na Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kwa sababu hafungi idadi kubwa ya magoli kama wananvyofanya wawili hao.
Pogba (22) anachukuliwa kama moja ya wachezaji wenye uwezo mkubwa dimbani akiisaidia Juventus kutetea taji lake la Seria 'A' na kuingia fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya.
Platini hakuishia hapo tu bali aliongeza kuwa ni mapema mno kumfananisha Pogba pamoja na Messi na Ronaldo huku akisita pia kukubali endapo kijana huyo atakuwa kama wawili hao hata kwa hapo baadaye.
"Pogba ni nyota kweli? hapana, nyota katika mchezo wa mpira wa miguu ni yule anayefunga mgoli mengi," Platini aliliambia RTL.
"Sijui lakini kama Pogba ni mchezaji ambaye anaweza kufikia walichokifanya Messi na Ronaldo. Wanafunga magoli 50 kwa msimu.
"Ni kitu cha kuvutia sana ukimuangalia pale anapopotea uwanjani halafu timu ikayumba, watu wote wanamgeuzia macho yeye akiwa kama ndio nguzo."
Pogba amefunga magoli 10 katika michezo 38 aliyocheza msimu huu akiwa na klabu yake ya Juventus.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video