Wakati Arsene Wenger akikanusha kutaka kumsajili Petr Cech,
wakala wa kipa huyo, Viktor Kolar amethibitisha kwamba Arsenal ni miongoni mwa
klabu tatu ambazo mlinda mlango huyo wa Chelsea
angependa kujiunga.
Kolar amesema klabu tatu ambazo Cech ana nia ya kwenda ni Manchester United, Arsenal na Paris
Saint-Germain.
Cech amekaa benchi karibu
msimu mzima baada ya kupoteza nafasi ya kwanza mbele ya Thibaut Courtois, na sasa
anafikiria kuondoka Stamford Bridge kutafuta timu atakayopata namba ya kudumu.
Wakati
hayo yakiendelea, kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amesisitiza kuwa kama
lingekuwa mikononi mwaka asingemruhusu kwenda klabu kubwa zenye wachezaji
wakubwa na ameweka wazi nia ya kumbakiza kipa huyo ambaye anamuheshimu kutokana
na uzoefu wake.
0 comments:
Post a Comment