Mashabiki
wameshindwa kuvumilia hali ya kusubiri mabondia kupanda ulingoni baada ya
waandaji wa pambano kati ya Francis Cheka dhidi ya bondia Kiatchai Singwancha
kuonekana wanachelewesha kwa makusudi mabondia waliondaliwa kuzichapa kwenye
mapambano ya utangulizi kinyume na ratiba ilivyokuwa ikielekeza.
Mashabiki
alimanusura waanzishe fujo kutokana na uvumilivu kuwashinda.
Mashabiki
hao waliojitokeza kwa uchache wameonekana kukasirishwa na kitendo hicho na
kuanza kumsaka ‘promoter’ wa pambano hilo lakini polisi imebidi waingilie kati
kutuliza rapsha zilizotaka kutokea.
Awali
ya yote, waandishi wa habari wametumia msuli kuingia kwenye ukumbi baada ya
walinzi waliokuwa mlangoni kuwazuia na kudai hawatambui uwepo wao mahali hapo.
Kitu hicho kiliwaudhi waandishi na wengine kuamua kususi pambano hilo na
kuondoka.
0 comments:
Post a Comment