GAZETI la leo jumapili la The Sun limechapisha stori maalumu kutoka kwa vyanzo vya karibu vya Mwanamitindo maarufu wa Urusi, Irina Shayk ambaye alivunja uhusiano wa mapenzi dhidi ya nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo.
Hata hivyo The Sun limeshindwa kujaa na nukuu kutoka kwa wawili hao (Ronaldo na Irina).
Mwanamitindo wa Urusi Shayk na 'supastaa' wa Real Madrid, Ronaldo walikuwa na mahusiano ya mapenzi kwa miaka mingi, lakini mahusiano yao yalivunjika mwanzoni mwa mwaka huu.
Irina Shayk kutoka hapo ana mahusiano na mwigizaji wa Hollywood, A-lister Bradley Cooper na anaonekana kufurahia mapenzi yao.
Lakini sasa ameamua kumwaga mchele akieleza kilichomfanya aachane au ampige chaga Ronaldo.
Kwa mujibu wa gazeti hilo la udaku, Cristiano Ronaldo alimsaliti Irina Shayk kwa kutembea na 'dazani' ya wanawake, yaani Ronaldo alizidi kuwa na michepuko.
Wakieleza zaidi namna Irina alivyobaini, The Sun wanasema Cristiano alikuwa anachati na wanawake wengi mno ambao walibainika kuwa wapenzi wake au michepuko yake na hali hii ikaamusha hasira za Irina.
Sasa imefahamika kwa mujibu wa ripoti ya The Sun kuwa Ronaldo ndiye aliachwa na Irina Shayk na sio yeye kumuacha mwanamitindo huyo.
Tazama nakala ya gazeti la The Sun chini likieleza stori hiyo
0 comments:
Post a Comment