Ukiwa ni wakati maalum kwa ajili ya wachezaji kuhama kwenda timu moja hadi nyingine na wengine kuboresha mikataba yao, kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Niyonzima kimsingi amekubaliana na Yanga kusaini mkataba mpya wa miaka miwili (2).
Hata hivyo Niyonzima bado hajasaini makaratasi, lakini makubaliano yameshafanyika kati ya pande mbili na kufikia muafaka.
Yanga inajidhatiti kusaini wachezaji kwa ajili ya msimu ujao ambapo watashiriki ligi ya mabingwa Africa na ikikumbukwe baadhi ya nyota wake wamehama klabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment