WAWAKILISHI pekee wa Tanzania
katika michuano ya kombe la Shirikisho
barani Afrika, Dar Young Africans leo wanashuka katika dimba la Anex Olympic de
Sousee, Tunisia kupambana na Etoile du Sahel katika mchezo wa marudiano wa
hatua ya 16 bora unaotarajiwa kuchezewa majira ya 3:00 kwa saa za Afrika mashariki.
Mechi ya kwanza iliyopigwa
wiki mbili zilizopita jijini Dar es salaam, timu hizo zilitoka sare ya 1-1 na
Yanga wanahitaji ushindi au sare ya kuanzia magoli 2-2 ili kusonga mbele.
Kama timu hizo zitatoka sare
ya 1-1 tena leo, basi dakika 30 zitaongezwa na ikishindikana kupata mshindi wa
jumla basi mikwaju ya penalti inatumika.
Wachezaji wa Yanga wana
morali ya hali ya juu kufanya vizuri leo na hapa ni kauli zao wakati wakiongea
na mtandao huu mchana huu:
MRISHO NGASSA: “Mazoezi yalikuwa ni mazuri, tumejiandaa
vizuri, hali ya hewa ni nzuri tu. Watanzania waweze kutuombea dua kwa wingi
tuweze kuibuna na ushindi. Tuko fiti wote kwa ajili ya mechi”
SIMON MSUVA: “Watanzania waiombee timu yao, tuweze kufanya
vizuri, kama wao waliweza kufanya vizuri kwetu wakapata goli hata sisi tunaweza
kupata kwao. Watanzania wawe na imani na timu yao, chochote kinaweza kutokea”
SALUM TELELA: “Mimi nashukuru Mungu naendelea vizuri, nipo
tayari kwa mchezo wa leo, hali ya hewa haiwezi kutuathiri kwasababu tulishawahi
kucheza mikoani na kupata matokeo mazuri licha ya kuwepo baridi. Watanzania
watuombee tuweze kupata matokeo mazuri katika mchezo wetu”.
Kwa upande wa kocha msaidizi, Charles Boniface Mkwasa
amethibitisha vijana wao kuwa na mroali ya hali ya juu na amesema: “Kwa ujumla
hali inaendelea vizuri, kama tulivyozungumza vijana wetu wanaonesha morali ya
hali ya juu ingawa kuna hali ya ubaridi kidogo, lakini wameweza kujiandaa,
nadhani tutakabiliana nao vizuri leo”.
Watanzania tuwe kitu kimoja, ingawa ni mbali, lakini tuko
pamoja nao, na tunafanya kwa ajili yao, wawe nyuma yetu, watusapoti ingawa si
rahisi kuwaona, lakini dua yao itatusaidia sana leo”
0 comments:
Post a Comment