Mshambuliaji wa Young Africans Mrisho Ngasa amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom mwezi Aprili kufuatia kuwapiku Amos Edward, Frank Domayo na Emmanuel Okwi baada ya kupata alama nyingi za jumla za mchezaji bora kwa kila mchezo.
Naye mchezaji James Mwasote Ambrose wa timu ya Tanzania Prisons FC amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Machi 2015 kufuatia kuwapiku wachezaji wengine waliokua wakiwania nafasi hiyo.
Jopo la maalum la makocha ambao hutafuta wachezaji bora kwa kila mchezo na kisha kujumlisha alama za mchezaji kwa kila mchezo na kumpata mchezji bora wa mwezi, ndio hufanya kazi ya kuchagua mchezaji bora kwa kila mwezi.
Kwa kuibuka wachezaji bora wa mwezi Machi na Aprili, James Ambrose na Mrisho Ngasa watazawadiwa fedha taslimu sh. milioni moja kwa kila mmoja kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodaom.
0 comments:
Post a Comment