Sunday, May 31, 2015

UONGOZI wa Ndanda fc umeachana na kocha wake, Meja Mstaafu, Abdul Mingange aliyeiongoza timu hiyo robo tatu ya msimu uliopita.
Mingange alijiunga na Ndanda fc mwanzoni mwa msimu uliopita akichukua mikoba ya Dennis Kitambi.
Mwanajeshi huyo msataafu amemaliza mkataba wa kuinoa Ndanda, lakini viongozi wa klabu hiyo hawajaona haja ya kumuongezea mkataba kwasababu hawajaridhishwa na kiwango cha timu yao.
Ndanda katika msimu wake wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara, 2014/2015 uliomalizika mei 9 mwaka huu walimaliza nafasi ya tisa wakijikusanyia pointi 31. 
Afisa habari wa klabu ya hiyo, Idrissa Bandali ameuthibitishia mtandao huu kuachana na Mingange.
Idrissa amesema tayari klabu hiyo imempata mrithi wake ambaye ni Jumanne Chale.
Chale aliwahi kuifundisha Prisons msimu wa 2013/2014, lakini alimanusra aishushe daraja kama uongozi usingemtimua na kumpata timu David Mwamwaja.
Chale alikwenda Rhino Rangers ya Tabora na kuishusha daraja, lakini Ndanda hawajazingatia hilo wakiamini bado ni kocha wa maana kwao.
Leo majira ya saa 1:00 usiku, Ndanda watatoa taarifa rasmi kuhusu mabadiliko hayo pamoja na mambo mengine yahusuyo klabu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video