Saturday, May 2, 2015

Na Kassim Mtolea
Uwanja wa Nangwanda sijaona mkoani Mtwara leo unatoa  hukumu kwa timu ya Ndanda fc kama itabaki ama itashuka kwenye mashindano ya ligi kuu msimu huu.
Timu hiyo ngeni kwenye ligi kuu inatupa karata yake ya ishirini na tano mbele ya "wanankurukumbi"timu ya Kagera sukari kutoka kule mkoani Kagera.
Akizungumza na MPENJA BLOG katibu mkuu msaidizi wa timu hiyo Seleman Kachele amesema kwa upande wao wapo kamili kupamba na wakata miwa hao.
"Tunajua Kagera ni wazuri na ni wakongwe katika ligi lakini tutahakikisha tunafanya kila liwezekanalo kuondoka na ushindi hii leo hapa nyumbani na kufufua matumaini ya kubaki ligi kuu kwa msimu ujao naamini tutapata ushindi hii leo dhidi ya wapinzani wetu hao".
Pia katibu huyo amewaomba mashabiki wa timu hiyo kuwa na utulivu kipindi hiki ligi inapoelekea ukingoni na kuwataka wapenzi na mashabiki pamoja na wanachama kuungana na kuwa kitu kimoja kuinusuru timu yao.
"Mwenendo wetu hauridhishi hata kidogo lakin hatupaswi kukata tamaa niwaombe mashabiki wapenzi na wanachama kuunganisha nguvu kwa pamoja ili kuisaidia timu yetu imalize salama michezo yake miwili iliyobaki ikiwa ni mchezo wa leo na ujao dhidi ya Yanga".Alisema Kachele.
Lakini wakati Ndanda wao wakisema hivyo kwa upande wao wakata miwa Kagera Sukari tayari wameshaingia mkoani humo na wapo tayari kwa kulipa kisasi mbele ya wamakonde hao.Kocha msaidizi wa timu hiyo Mrage kabange amesema wala hatishwi na tambo za wenyeji wao hao.
"Waache waongee ni haki yao maana wapo nyumbani kwao pia ni uwanja wao kwahiyo wanayo sababu ya kuzungumza lakini sisi kilichotuleta huku ni alama tatu na wala sio maneno tupo tayari kwa mchezo na watu watajua kitakachotokea hapo hapo baadaye we nitafute baada ya mechi nikupe matokeo".Alihitimisha Kabange.
Huo utakuwa ni mchezo wa pili kwa timu hizo kupamba katika ligi kuu ambapo katika mchezo wa awali uliipigwa kwenye dimba la CCM Kirumba Mwanza kama uwanja wa nyumbani  timu ya Kagera Sukari ilikubali kichapo cha goli mbili kwa moja na kupelekea timu hiyo kukimbilia mkoani Shinyanga kwwnye uwanja wa Kambarage huku kambi ya timu ikibaki jijini Mwanza

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video