NDANDA FC wamefufua matumaini ya kubaki ligi kuu
soka Tanzania bara baada ya jioni hii kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya
Wakata miwa wa Kagera Sugar kwenye mchezo uliopigwa Nangwanda Sijaona.
Goli la
kwanza la Ndanda fc limefungwa na Dideon
Benson dakika ya 15 na la pili limetiwa kambani na Nassor Kapamba dakika ya 45.
Mechi hiyo ambayo ambayo Ndanda walikuwa na uchu
wa ushindi, Kagera Sugar wenye pointi 31 mpaka sasa hawakuonesha makeke kama
walivyozelewa na kuwashangaza mashabiki waliojitokeza uwanjani.
‘Mtwara Kuchele’ Ndanda fc
wamefikisha pointi 28 na angalau kufufua matumaini wakisubiri mechi ya Mei 9 mwaka huu dhidi ya Yanga.
Kocha msaidizi wa Ndanda fc, Ngawina Ngawina amesema mechi na Yanga ni ngumu lakini wanaisubiri kwa hamu ili kuwaonesha Watanzania uwezo waliokuwa nao.
Mechi ya kwanza uwanja wa Taifa, Yanga na Ndanda walitoka suluhu.
0 comments:
Post a Comment