Friday, May 22, 2015

Bilionea Aliko Dangote
Uongozi wa Ndanda FC unajipanga kukutana na bilionea namba moja barani Afrika, Aliko Dangote kwa ajili ya kumuomba kuwa mmoja wa wadhamini wa juu katika timu hiyo kabla msimu ujao haujaanza.
Salehjembe ameripoti kwamba  mwenyekiti wa Ndanda FC, Hamad Omari alisema licha ya kuwa na udhamini wa Kampuni ya Binslum na Big Tanzania, lakini wanajipanga kumuona tajiri huyo anayemiliki kiwanda cha saruji kwenye mkoa wao.
“Tunafikiria kufanya mikakati ya kuweza kukutana naye ili aweze kuwa mdhamini mkuu kwenye timu yetu ambayo imenusurika kushuka daraja.
“Unajua tangu ligi imemalizika bado hatujakaa kuweza kujadili hayo mambo na kama ataweza kukubali basi litakuwa ni jambo jema kwa sababu fedha zinazotolewa na wadhamini wa ligi hazikidhi mahitaji ya timu kwa msimu wote, sasa lazima njia nyingine zitumike kuhakikisha tunakuwa vizuri zaidi msimu ujao,” alisema Omari.

Dangote, raia wa Nigeria, kwa sasa ana kiwanda cha saruji mkoani Mtwara ambako timu hiyo inatokea, anakadiriwa kuwa na utajiri wa pauni bilioni 10.4 (shilingi trilioni 2.7) na hivi karibuni alitangaza nia ya kuinunua Klabu ya Arsenal ya England.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video