#
|
Team
|
GP
|
W
|
D
|
L
|
GF
|
GA
|
GD
|
PTS
| |
1
|
37
|
25
|
9
|
3
|
70
|
31
|
39
|
84
| ||
2
|
37
|
23
|
7
|
7
|
81
|
38
|
43
|
76
| ||
3
|
37
|
21
|
9
|
7
|
67
|
35
|
32
|
72
| ||
4
|
37
|
20
|
9
|
8
|
62
|
37
|
25
|
69
| ||
5
|
37
|
18
|
8
|
11
|
51
|
42
|
9
|
62
| ||
Kushushwa daraja kwenye ligi kuu ya Uingereza sio jambo baya kuliko yote. Ligi daraja la kwanza (Championship) ni sehemu nzuri sana, mtu anaweza kutegemea timu iliyoshushwa itashinda mechi nyingi ikiwa hapo chini kuliko ilivyofanya kwenye Ligi Kuu. Kitu cha kuangalia ni kutokosa uangalizi na mwelekeo kama Leeds na Portsmouth. Cha kuzingatia ni matumizi mazuri ya pesa kiasi cha Paundi 60 Mil (zaidi ya Bilioni 160, shilingi za Tanzania) ambacho timu inapewa pindi inaposhuka.
Lakini tukija moja kwa moja kwenye wikiendi hii ambayo ni ya mwisho kwenye Ligi Kuu kwa msimu wa 2014-15, ngoja tuwe wawazi, kushushwa daraja ni jambo baya kuliko yote. Kesho Newcastle na Hull watakuwa wametawaliwa na mawazo ya mmoja wao kuungana na Burnley pamoja na QPR kushushwa daraja. Wakati Hull akiwa mwenyeji wa Man United, Newcastle yeye atakuwa mwenyeji wa West Ham pale St James’ Park. Wasiwasi utakuwa mkubwa sana baina ya timu hizi mbili. Mechi zitachezwa muda mmoja na kama ilivyo kawaida ya siku ya mwisho kamera zitakuwa zikichukua picha za mashabiki wakitafuna kucha zao hadi mifupa. Hull wanahitaji kushinda kwa gharama yoyote ile lakini hata kushinda inawezekana kusiwanusuru kuepuka panga la kushushwa chini kwa sababu Newcastle wamewazidi pointi mbili hiyo inawafanya hatima yao itegemee matokeo ya Newcastle kwa kiasi kikubwa.
Kwa Hull City, rekodi hazioneshi picha nzuri kwao. Steve Bruce, kocha wa Hull City hajawahi kuifunga klabu yake ya zamani, Manchester United katika miaka yake yote 17 kama kocha. Katika mechi 21 amepoteza mechi 17. Mechi hizo zinajumuisha timu alizozifundisha hapo nyuma kama Birmingham, Wigan, Sunderland pamoja na timu yake ya sasa Hull City, kushindwa kwake kuifunga timu yenye mafanikio zaidi katika ligi kuu hakuleti picha nzuri kwa Hull City. Kitu kibaya zaidi kwa Steve Bruce ni Hull City kuwa katika nafasi hii wakati wametumia Paundi 69 Mil katika miaka miwili iliyopita. Lazima watu wawajibike wakati huu msimu unaisha.
“Labda nawadai kitu United baada ya kuumia goti langu, nyonga na enka”, alisema Bruce kuelekea mechi ya Jumapili hii, katika hali ya utani.
Matumaini mengine ya Hull City kushinda mechi yanatokana na Manchester United kufanikiwa kurudi kwenye ligi ya mabingwa Ulaya na pengine labda hawatakaza uzi sana katika mechi hii. Lakini matumaini ya Hull katika hili pia, yanapata pigo lingine, Man United inaweza kutafuta ushindi mkubwa sana dhidi yao kwa matumaini kuwa labda Arsenal itapoteza mechi yake na West Brom hivyo wao kupata nafasi ya tatu itakayowapeleka moja kwa moja kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa.
Newcastle wao wataingia katika mechi yao dhidi ya West Ham wakiwa makini sana ili wasije wakashuka daraja kwa staili ya aina yake. Sare waliyoipata wiki mbili zilizopita iliongeza uzito mkubwa sana kwenye kikosi hicho cha John Carver huku yeye mwenyewe akijiita “Kocha Bora kwenye Ligi Kuu” kwa sababu ilimaliza mfululizo wa kupoteza mechi nane.
Lakini huku wakiwa na matumaini ya kufanya vema kwenye mechi inayofata, Newcastle ilijikuta ikifungwa na timu iliyo mkiani mwa Ligi Kuu, QPR. Carver alisema moja ya sababu za wao kupoteza mechi ile ni hali ya hewa ambayo ilikuwa ya joto.
Kwa upande wa wapinzani wao, kutakuwa na mtu anaitwa Sam Allardyce, kocha aliyeifundisha Newcastle kwa miezi nane, kabla ya kukiri kushtushwa na kufukuzwa kwake mwaka 2008. Kuelekea kwenye mechi hiyo, Big Sam alisema: “Huwezi kuonesha huruma kwa yeyote yule, kwa sababu hakuna mwenye huruma kwako” Inategemewa hii itakuwa mechi ya mwisho kwa Big Sam, kama kocha wa West Ham, kwa sababu hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa juu ya kuongezewa mkataba mpya huku alionao sasa ukiisha wakati wa majira haya ya joto (kwao – Ulaya). Fikiria itakwaje kama mchezaji wa zamani wa Newcastle, na nahodha wa sasa wa West Ham, Kevin Nolan atafunga goli lake la 100 kwenye Ligi Kuu kabla ya kumkimbilia Sam Allardyce na kumkumbatia

0 comments:
Post a Comment