Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amemaliza muda wake
KATIBU mkuu wa kamati ya
uchaguzi ya Yanga, Francis Kaswahili jana amekaririwa na vyombo vya habari
akisema uchaguzi mkuu wa Yanga SC
utafanyika Julai 12, mwaka huu katika ukumbi ambao utatajwa baadaye.
Taarifa hiyo
ilifafanua kuwa fomu za wagombea zitaanza kutolewa Mei 17, mwaka huu kwa
kuzingatia ratiba.
“Jambo hili ni la
kikatiba na wala halina mjadala, tunataka Yanga iwe na viongozi ambao
watatokana na utashi wa Wanayanga ni matumaini ya kamati ya uchaguzi kwamba
hapatatoka mtu mwingine wa kutaka kuvunja misingi ya katiba”. Kaswahili
alikaririwa na Bin Zubeiry.
Lakini katika hali ya
kushangaza, jioni ya leo mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Yanga,
Mwanasheria, Alex Mgongolwa ameibuka na kusema kwa mujibu wa katiba ya Yanga,
mwenye wajibu wa kutangaza uchaguzi ni mwenyekiti na sio katibu mkuu ambaye
hajui kama ni Francis Kaswahili.
“Kwa mujibu wa katiba,
mikutano ya namna hiyo lazima iweze kuratibiwa na sekretarieti, halafu
mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ndiye anaitisha mkutano mkuu. Kwa mujibu wa
katiba za wanachama wa TFF, katibu hawezi kuitisha mkutano wa uchaguzi na pia
sina hakika kama yeye ndiye katibu mkuu kwasababu kikatiba katibu mkuu lazima
atoke kwenye sekretarieti, nayeye (Kaswahili) sio mjumbe, hana mamlaka yoyote”.
Mgongolwa amekaririwa na kituo cha redio cha E-fm usiku wa leo.
Mgongolwa amesisitiza kuwa
mkutano aliotangaza kaswahili ni batili na hana mamlaka ya kuitisha wala
kutangaza huo mkutano.
Hata hivyo kuhusu uchaguzi wa
Yanga, Mgongolwa amesema:“Taarifa ambazo nimezipata na ninasubiri mawasiliano
kutoka sekretarieti ni kwamba kamati Yangu itakutana wiki ijayo kupanga tarehe
ya uchaguzi mkuu wa Yanga”.
0 comments:
Post a Comment