Na Ramadhani Ngoda
Meneja
wa Aston Villa, Tim Sherwood ameonesha kukata tamaa ya kumbakisha mshambuliaji
wake raia wa Ublgiji Christian Benteke kutoikana na kipengele cha mkataba wake
kinachomruhusu kuondoka endapo timu itafika bei ya pauni million 32.5.
Sherwood
ana uhakika kuwa Mbelgiji huyo anataka kubaki Villa Park lakini amekiri itakuwa
vigumu kutokana na kipengele hicho kilichopo kwenye mkataba wake aliosaini miezi
miwili iliyopita, anaweza kuondoka kama kiwango hicho cha fedha kitafikiwa na
timu inayomhitaji.
“Kuna
kipengele cha bei katika mkataba wake hivyo itakuwa vigumu kumzuia kuondoka
pale atakapohitaji. Timu yoyote inayomuhitaji inabidi kufika bei hiyo
vinginevyo itakuwa ngumu kwa sababu hatutaki kumpoteza,” alisema Sherwood.
Christian Benteke(kulia) akiwa na kocha wake Tim Sherwood(kushoto) |
Vilabu
vya Arsenal, Chelsea, Liverpool na Manchester United tayari wameonesha nia ya
kusaka dole gumba la mshambuliaji huyo aliyetoa mchango mkubwa kwa klabu hiyo
ikiwemo kufika fainali ya kombe la FA watakayokipiga dhidi ya Arsenal katika dimba
la Wembley wikiendi hii, pia akifunga mabao 12 katika mechi 12 za mwisho.
Sherwood
hakusita kumuonya nyota wake wake huyo juu ya kukurupuka kuhama Villa Park
kabla ya michuano ya EURO 2016 kutokana na kutokuwa na uhakika wa namba ya
kudumu kwenye klabu atakayohamia na
kuhatarisha nafasi yake kwenye timu taifa.
“Ni
mashindano ambayo Ubelgiji ni moja ya timu zinatazamiwa kushinda, kucheza Aston
Villa hakuhatarishi yeye kuwa chaguo la kwanza Ubelgiji. Arudi kwenye historian
a aangalie nini kiliwakuta waliowahi kuhama”
Christian Benteke(24)
mzaliwa wa Kongo Kinshasa, aliyewahi kuvichezea pia vilabu vya Genk, Standard
Liege, Kortrijk na Mecheleen zote za Ubelgiji, alisajiliwa na Aston Villa mwaka
2012 akitokea Genk ya nyumbani kwao kwa uhamisho wa pauni milioni 7 tu,
ameshaichezea Villa mechi 88 na kufanikiwa kufunga mabao 42 mpaka sasa
0 comments:
Post a Comment