Wednesday, May 20, 2015

MOJA ya watu wanaoipenda Yanga na kuumia pale inapofanya vibaya kwa maana ya timu nzima au mchezaji mmoja mmoja, ni 'Admin' wa ukarasa maarufu katika mtandao wa kijamii wa facebook wa ;Naipenda YANGA', Bwana Hissan Salum.
Leo hii katika ukarasa wake ambao unatoa habari maalumu za Yanga ame-post maoni yake kuhusu kushuka kwa kiwango cha mshambuliaji wa kimataifa wa Liberia anayekipiga Jangwani, Kpah Sherman.
Salum amedai Sherman anapenda sana anasa tofauti na wachezaji wengine wa kimataifa kama vile Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Amissi Tambwe.

UJUMBE WAKE AMBAO MTANDAO HUU UMEHAMISHA KUTOKA KATIKA UKURASA HUO NI HUU HAPA CHINI;
"Kpah Sean Sherman japo amekuwa na msimu mbovu tofauti na ilivotegemewa lakini amekuwa kipenzi cha Wana Yanga,kiwango alichokionyesha siku ya mtani jembe ikiwa ni siku moja tu toka awasili nchini kiliwavutia wengi na akateka hisia zetu!taaratibu akaanza kuflop akawa anacheza katika kivuli cha kiwango chake tulichokiona mwanzo,tuna benchi makini sana ambalo hawana kubebana wala kumuogopa mtu nao bila ajizi wakaanza kumpiga benchi na mara nyingine kumtupa jukwaani kabisa, , chanzo kikubwa cha kuporomoka kiwango ni mchezaji wetu kuendekeza sana anasa, mara nyingi huwa anaibiwa vitu nyumbani kwake wanaomuibia ni wanawake!hii ni Bongo Daslam bana shabiki humtafutia mchezaji wake mwanamke au kumnunulia pombe,nchi iliyojaa uswahili na siasa katika soka inahitaji akili kubwa ya kujitambua ili ubaki katika kiwango chako ulichokuja nacho siku unatua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere!angalia maisha wanayoishi Haruna Niyonzima,Mbuyu Twite,Amiss Tambwe ni tofauti kabisa na maisha ya Kpah Sherman. . Klabu yetu imetoa pesa kuwasajili na kuwalipa mishahara minono tunaomba ziteendeeni haki pesa hizo, tunasajili nyota wawe msaada kwa klabu lakini matokeo yake upuuzi tu!benchi limempa muda mwingine wa kuthibitisha ubora wake la sivyo tutaachana naye, , hatuingilii maisha yake binafsi au mahusiano yake kimapenzi na Agnes Masogange la hasha sisi tunataka afanye kazi iliyomleta tu, hayo mengine afanye sana ila tu magoli aifungie klabu yetu hicho ndo tunataka wana Yanga hiyo ndio kiu yetu tushangilie magoli.Likizo njema Kpah Sherman ni muda wako kufikiria wapo ulipojikwaa tuna tegemea utajirekebisha na kutupa furaha wananchi.
Admin Hissan Salum.".

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video