TANZANIA Prisons wataikaribisha Mbeya City fc katika mchezo
wa ligi kuu soka Tanzania bara utaopigwa kesho kuanzia saa 10:00 uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya.
Mbeya City waliopo nafasi ya nne kwa pointi 31 wanazihitaji
pointi tatu ili kujiimarisha katika nafasi hiyo, wakati Prisons wanaoshika
nafasi ya 12 wakijikusanyia pointi 25 wanataka ushindi ili kujiweka mazingira
ya kutoshuka daraja.
Kocha mkuu wa Mbeya
City Juma Mwambusi amesema: “Tumejiandaa vizuri kesho kuhakikisha tunapata
pointi tatu muhimu kesho”.
Kocha huyo pia ameeleza kwanini kikosi cha Mbeya City
kimesuasua msimu huu tofauti na msimu uliopita ambao walimaliza ligi wakiwa
nafasi ya tatu.
“kiujumla kila mtu anakuwa na changamoto zake kuanzia kwa
utawala, mpaka wachezaji, unajua msimu uliopita tulifanya vizuri na kila mtu
akawa anajiona yuko bora, katika maandalizi viongozi walijisahau, program ya
mwalimu haikufuatwa kama zamani, walikuwa wanaona kama wana kikosi bora wakati
kikosi bora lazima uwe na maandalizi makubwa sana “. Amesema Mwambusin na
kuongeza: “Lakini tukakaa chini na kuona wachezaji ambao tunaweza kuwatoa na
kuleta wachezaji wengine katika dirisha dogo na wamekuja kubadilisha hali ya
kikosi”
KWANINI MBEYA CITY IMEKUWA MTEJA KWA YANGA?
Mwambusi anasema: “Mikakati yetu mikubwa ni kushinda,
tuliweza kuwafunga Simba hapa na tungeweza kuwashinda hata Yanga kule Dar es
salaam, lakini kama unavyojua tukicheza mchezo uwanja wa Taifa na Yanga lazima
tupate kadi nyekundu, hii si sawa, tukibaki 11 kwa 11 tunaweza kufanya vizuri.
Simba tumecheza nao hatujawahi kupata kadi nyekundu na tumeweza kuvuna pointi.
Tunaangalia mbele na michezo hii ya mwisho waamuzi wawe makini”.
Hata hivyo Mbeya City msimu huu ilifungwa magoli 3-1 dhidi
ya Yanga uwanja wa Sokoine ikiwa na wachezaji 11.
0 comments:
Post a Comment