Saturday, May 30, 2015

Na George Mganga,
Kijana mdogo wa miaka 20,21 au 22 unasajiliwa kwa kitita cha 50 Milions! Mshahara wa 2 au 1.5 milioni katika mkataba wa miaka miwili.
Humo kuna posho mbalimbali achilia mbali timu ikifanya vizuri kuna bonus na chenji nyingi tu toka kwa wachezaji wafurukutwa. Dah!
  Unajikusanyia takribani milioni 89 hadi 100 katika hiyo kandarasi yako.
  Kilichonifanya niandike hili ni lawama zisizo za msingi kwa vilabu vyetu hapo baadaye maisha yanapo wageukia wachezaji wetu hususani ligi kuu.
  Badala ya kunyanyua mikono kwa Mola na kuanza kujijenga basi wengi wenu mnainua mikono yenu kutimiza zile ndoto hasi za ujana.
  Unatamani kuufuata mgongo wa Diamond kwa kila anachofanya. Kumbuka yeye anaweza kuimba hata akiwa na miaka 40 lakini umri wa soka hauzidi miaka 15 kama ulianza kwa umri stahiki wa miaka 20.
Na si miaka hiyo yote utang'ara ukiwa Azam , Simba au Yanga vilabu ambavyo vina usajili wenye pesa nyingi na mishahara mizuri.
  Hapa juzi mchezaji analalamika hana hata godoro achilia mbali pa kulala dah!
   Acheni masihara wadogo zangu. Mishahara na pesa mnazo chukua katika usajili wenu , wazazi wetu na wenu inawachukua si chini ya miaka 20 hadi 30 kama mafao ya uzeeni.
  Watu mtaani wanatengeneza maisha kwa mishahara ya sh 320,000 kwa mwezi bila allowance za maana.
Mkiwa katika mabasi ya klabu si huwa mnawaona wamachinga njiani ?! Au mama ntilie? Kwa kidogo walicho nacho wana jenga na kusomesha kwa nini nyinyi mnachezea maisha kwa starehe zisizo na maaana?!
  Mpira unakwisha, mawazo na maradhi yanaanza kuwasumbua mnapitisha mabakuli mitaani.
  Hapana bwana, wenzenu walifanya makosa hayo na wengine si makosa bali enzi zao soka lilikuwa hakuna pesa kama sasa!
  Amkeni jamani!.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video