Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amechaguliwa kuwa kocha bora wa msimu ligi kuuu nchini Uingereza akiungana na mchezaji wake Eden Hazard ambaye alichukua tuzo ya mchezaji bora wa msimu.
Mourinho ameisaidia Chelsea kutwaa taji la kwanza la ligi kuu nchini Uingereza baada ya kulikosa kwa takribani miaka mitano huku wakivunja rekodi ya kukaa kileleni kwa kukaa siku 274.
Hii ni mara ya tatu kwa Mreno huyo kutwaa taji hilo pamoja na kutajwa kama kocha bora wa msimu. Aliwahi pia kutwaa mwaka 2004-05 and 2005-06.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho akisherehekea kushinda tuzo ya kocha bora wa ligi kuu nchini Uingereza.
0 comments:
Post a Comment