Uongozi wa Simba umepokea maombi ya makocha kutoka mataifa
mbalimbali kwa ajili ya kumrithi Mserbia, Goran Kopunovic, kati ya hayo yumo
Mmarekani mmoja.
Timu hiyo, hivi sasa ipo kwenye mchakato wa mwisho wa
kukamilisha mchujo wa kumpata mbadala wa Kopunovic atakayekinoa kikosi hicho
baada ya kuachana na Mserbia huyo ambaye walishindana naye dau kufuatia
kumalizika kwa mkataba wa muda mfupi aliosaini awali.
Gazeti la michezo la Championi limemnukuu Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, akisema Mmarekani huyo yupo kwenye orodha ya majina ya makocha wanaotaka kurithi
kibarua cha Kopunovic.
Kaburu alisema kuwa, pia wamepokea maombi ya kocha kutoka
nchini Asia ambaye anatimiza idadi ya makocha 100 wanaotaka kuifundisha timu
hiyo.
“Ipo kamati husika inayohusika na mchakato huo wa kumpata
kocha mpya atakayeifundisha Simba, hadi hivi sasa imefikia idadi ya makocha
100.
“Makocha wa mataifa mbalimbali wamejitokeza kiukweli, yupo
kutoka Marekani na Asia ambao wote tunaamini ni wazuri, yupi atakayekabidhiwa?
Tuiachie kamati inayohusika na mchakato huo,” alisema Kaburu.
0 comments:
Post a Comment