Na Bertha Lumala, Dar es Salaam.
KOCHA wa JKT Ruvu Stars, Felix Minziro, amesema kutofanya vizuri kwa timu yake Kwenye ligi kuu ya Bara msimu uliopita kulitokana na wachezaji wengi kwenda mafunzoni.
Minziro, kocha wa zamani w Yanga, ambaye timu yake ilishika nafasi ya nane, amesema wachezaji wake muhimu walikwenda katika mafunzo ya jeshi mwanzoni mwa mwaka na hivyo kupelekea kufanya vibaya tofauti na raundi ya kwanza.
Minziro amesema amejipanga kutafuta wachezaji wazuri kwa ajili ya msimu ujao, tofauti na miaka ya nyuma ambapo timu ilikuwa ikichukua wengi kutoka mchangani.
"Wachezaji wa kutoka mchangani, huwiwa vigumu kuendana na kasi ya ligi kuu ya Bara," amesema Minziro.
Sera ya kusajili wachezaji wa mchangani, hata hivyo, ilikuwa na lengo la kutoa nafasi za ajira ndani ya Jeshi la Kujenga Taifa linalomiliki timu hiyo, alisema Minziro.
“Ukweli sijafurahia hata kidogo kushika nafasi ya nane ambayo inaniumiza kichwa na timu yangu imefanya vibaya ni kutokana na wachezaji sita kwenda katika mafunzo ya jeshi na kubaki na wachezaji ambao viwango vyao ni vya kawaida tu,” alisema Minziro.
“Kusajili kwangu wachezaji wa mchangani ni kutokana na vijana wengi kutokuwa na ajira wakati wana uwezo wa kuonyesha vipaji vyao kwa kupitia soka na hivyo kupata nafasi ya ajira katika jeshi.”

0 comments:
Post a Comment