NDANDA FC inaburuza mkia katika msimamo wa ligi kuu ikiwa na
pointi 25 baada ya kushuka dimbani mara 24 na kesho jioni inacheza mechi muhimu
dhidi ya Kagera Sugar fc uwanja wa Nangwanda Sijaona kabla ya kumalizia msimu
na Yanga mei 9 mwaka huu katika uwanja huo.
Wakati timu hiyo inakabiliwa na michezo hiyo migumu, kocha
mkuu, Meja Mstaafu Abdul Mingange amebaki Dar es salaam kuendelea na kozi ya
ukocha na kwa maana hiyo msaidizi wake Ngawina Ngawina ataongoza benchi la
ufundi.
“Niko Dar es salaam kwenye kozi hapa TFF, timu yangu
imeondoka leo kwenda Mtwara. Nina wasaidizi wawili ambao nawaamini kabisa,
haina shaka, kwanza wachezaji wanajitambua na wamefanya mazoezi wakiwa na mimi
hapa Dar , walishafungwa mechi moja nyumbani wakiwa na mimi, tulifungwa na
Simba”. Amesema Mingange na kusisitiza: “Sijakata tamaa, ndio maana katika
mpango wangu timu ilikuwa Dar es salaam, timu imeondoka leo, hii yote ni
kuisaidia timu isishuke Daraja”.
0 comments:
Post a Comment