Wakati Manchester United na timu nyingine zikihangaika kutafuta wachezaji, The Special One, Jose Mourinho anasema yeye atakua busy na taulo lake beach na kuogelea.
“Nategemea kuwa busy nikitembea kutoka kwenye mchanga na kwenda kwenye maji na kuogelea kidogo, then narudi kwenye jua tena. Hicho ndicho kitu ambacho nitakua nafanya sehemu mbalimbali”
“Nakipenda kikosi changu sana, kuna wachezaji wenye umri mdogo na nafasi ya kuongeza uwezo wao. Nipo kwenye nafasi tofauti na msimu uliopita, nilikua nauza sana wachezaji lakini kwasasa hivi nina furaha na pia nawaweka wachezaji wangu. Lengo la msimu uliopita lilikuwa ni kuuza na kununua wachezaji wapya. Lakini lengo la sasa hivi ni ku-keep hiki kikosi na kukiendeleza zaidi”.
Jose aliongeza zaidi kwamba hatakuwa busy kusajili wachezaji wapya kwenye kipindi cha usajili kikifika.
0 comments:
Post a Comment