Piet de Mol
GORAN Kopunovic bado
anaihangaisha Simba kuhusu kusaini mkataba mpya na aliahidi kutoa jibu jana
ijumaa, lakini bado amekuwa mgumu kuweka wazi kama amekubali au la! kuendelea na
kibarua chake Msimbazi.
Sababu inayofanya Simba
washindwane na Kopunovic mpaka sasa ni
Mserbia kutaka mshahara mkubwa wa dola za Kimarekani elfu tisa (9,000) sawa na
shiloingi milioni 18 za Kitanzania.
Pia anataka dau la kusaini la
dola za kimarekani elfu hamsini (50,000) sawa na shilingi million 100 za
Kitanzania.
Siku za karibuni, mwenyekiti
wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe alikaririwa na vyombo vya
habari akisema wanasubiri maamuzi ya Kopunovic ambaye kwasasa yuko likizo
Hungary na kama atakataa kukubali ofa yao basi watatafuta kocha mwingine
kurithi mikoba yake.
Hans Poppe na viongozi
wenzake kwa siku nzima ya jana walikuwa wanasubiri jibu la Kopunovic, lakini
mpaka usiku hakukuwa na taarifa yoyote kutoka kwa kocha huyo mwenye mbwembwe
nyingi anapoiongoza timu yake.
Hata hivyo taarifa mpya
iliyotolewa na Bin Zubeiry asubuhi ya
leo inasema kocha Mbelgiji, Piet de Mol atatua Dar es Salaam Mei 21, mwaka huu kwa ajili ya mazungumzo ya
kuifundisha Simba SC, lakini kutua kwa kocha huyo kutategemea na msimamo wa
mwisho wa Simba SC juu ya Goran.
Kwa mujibu wa mtandao wa Wikipedia, De Mol mwenye umri wa miaka 60 ana uzoefu mkubwa wa kufundisha
soka Afrika, Asia na Ulaya na alikuwa nchini Ghana akifanya kazi ya Mkurugenzi
wa Ufundi wa akademi mjini Kumasi. Pia alifanya kazi
na Asante Kotoko. Pia alifundisha timu ya kwao Ubelgiji, Dubai, Qatar na China.
Alikuwa kocha Msaidizi wa AA Gent kuanzia mwaka 1997 hadi 2001.
0 comments:
Post a Comment