Thursday, May 21, 2015

MDAU wa soka, Hissan Salum Iddi, ambaye ni 'admin wa ukurasa maarufu kwenye mtandao wa facebook wa 'Naipenda YANGA' leo amekuja na maoni yake akisikitikia namna Taifa Stars ilivyohatarisha dili la Mrisho Ngassa na Simon Msuva kucheza soka la kulipwa Afrika kusini.
Hii inatokana na Stars kuvurunda katika mechi mbili za kwanza za kundi B katika michuano ya Cosafa.
Stars chini ya Mart Nooij ilifungwa mechi ya kwanza 1-0 na Swaziland na jana usiku imekula 2-0 kutoka kwa Madagascar.
Siku za karibuni, Ngassa alisaini mkataba wa miaka minne (4) kuitumikia Free State Stars inayoshiriki ligi ya 'Sauzi' wakati Msuva yeye aliripotiwa kufuzu majaribo katika timu ya huko huko ya Bidvest Wits inayocheza ligi kuu.
Lakini mawinga hao wawili wa Tanzania wamechemsha katika mechi za Cosafa na kuzua wasiwasi kwasababu wanafuatiliwa kiukaribu.

Bwana Hissan Salum Iddi anasema:

"Bila shaka mashabiki pamoja na viongozi wa Free State(timu mpya ya Ngassa) kiasi fulani wameingiwa na hofu juu ya kiwango cha Ngassa, lazima wanamfuatilia katika michuano hii ya COSAFA ili waone nini atakachowafanyia baada ya usajili huo. 
Walitegemea Ngassa aibebe Taifa stars dhidi ya vibonde Swaziland na Madagascar, hiyo ndio ilikuwa furaha yao kushuhudia kijana wao mpya akipiga mpira mwingi.
Sioni uhai tena wa dili la Simon Msuva kwende Bidvest Wits, kupitia michuano hii, waliendelea kujiridhisha na kujiuliza mara mbili mbili!je watume Maombi kumnunua?? 
Bila shaka yoyote hilo dili halipo tena,wamemshuhudia kijana huyo akiboronga dhidi ya mabeki dhaifu wa Swaziland na Madagascar,mfungaji bora mwenye magoli 17 lakini hata goli la offside hajafunga.
Michuano hii imetoa hukumu na taswira mbaya kuhusu ligi yetu. Ni aibu kuiangalia nchi yetu ikicheza vile na usitarajie wachezaji wako wauzike nje kwa kiwango kile.
Unapowasifia Ngassa na Msuva ni vema usisahau kuelezea ufanisi wa Salum Telela na Haruna Niyonzima au Said Makapu katika kuwachezesha Ngassa/Msuva.
Kocha wa Taifa stars ametoa hukumu mbaya dhidi ya Ngassa na Msuva huko ugenini, nahisi vichwani mwao kadri mpira ulivokuwa unaendelea walikuwa wakiwakumbuka Haruna Niyonzima na Salum Telela au Makapu au spidi ya Juma Abdul upande wa kulia pamoja na zile krosi zake maridadi.
Mara nyingi makocha wengi duniani wa timu za taifa hutembelea nyota ya klabu yenye mafanikio katika nchi husika,tumeshuhudia timu ya Barcelona ikitawala kikosi cha Spain hivo kumrahisishia kazi Del Bosque, au kule Ujerumani kikosi cha Bayern katika taifa lao!hii huwasaidia wachezaji kuwa na chemistry nzuri kwani wanakuwa wamecheza pamoja katika klabu. . 
Mart Nooij ameshindwa kusafiria nyota ya babu Hans van Pluijm!ile mipasi na spidi ya Yanga angeikopi kisha kuipestia timu ya Taifa,beki ya kulia Juma Abdul kama kawaida angesaidiana na Simon Msuva upande wa kulia au katikati angemweka Salum Telela aliyewafunika viungo ghali wa Etoile du sahel awachezeshe Ngasa na Msuva matokeo yake anatuwekea Erasto Nyoni!
Mart Nooij umetuabisha na kuwaibisha wachezaji wetu, kazi kubwa Hans van Pluijm alikwishaifanya ya kukuandalia wachezaji walio fit na chemistry nzurI ambao wangeweza kukubeba, jeuri yako umeifanya timu icheze ovyo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video