Israel Mujuni (katikati)
WAAMUZI
wanne (4) wa Tanzania wameteuliwa na Shirikisho la soka barani Afrika, CAF, kuchezesha mechi namba 8 ya kuwania kufuzu
fainali za mataifa ya Afrika, Afcon 2017 baina ya Uganda na Botswana.
Mwamuzi
wa kati katika mechi hiyo itayopigwa Juni 13 mwaka huu mjini Kampala, Uganda,
ameteuliwa Mtanzania Israel Mujuni Nkongo.
Watanzania
wengine watakaochezesha mechi hiyo na nafasi zao kwenye mabano ni John Longino
Kanyenye (mwamuzi msadizi namba moja), Josephat Deu Bulali (mwamuzi msaidizi
namba mbili) na Martin Eliphas Sanya (mwamuzi wa akiba).
Kamishina
wa mechi hiyo atakuwa Julius Elly O. Mukolwe kutoka Kenya.
0 comments:
Post a Comment