Na Ramadhani Ngoda
Licha
ya Angel Di Maria kuwa na msimu mbovu na kuishinmdwa kuwapa mashabiki wa United
kile walichotarajia, Kiungo wa zamani wa klabu hiyo, Paul Scholes ameibuka na
ksema kuwa Di Maria ni aina ya mchezaji ambaye Manchester United inamuhitaji
kwa sasa.
Di
Maria ambaye alisajiliwa kutoka Real Madrid kwa ada ya uhamisho ya pauni
milioni 59.7 amekuwa akihaha kuzoea maisha ya ligi kuu England, hali iliozua
shaka kwamba anaweza kuondoka Old Trafford majira ya kiangazi.
Scholes
ameonekana kumkingia kifua winga huyo na kumtaja kama mchezaji wa aina ya
kipekee ambaye United wasithutu kumwachia na atakuwa na mchango mkubwa msimu
ujao wa ligi na ligi ya mabingwa barani Ulaya.
“Ni
mwanzo mzuri, lakini kwa pauni milioni 59.7, tulitaraji angeipa United zaid
Zaidi ya hiki,” alisema Scholes.
Manchester
United wametimiza lengo la msimu kwa kushika nafasi ya nne na kurejea kwenye
michuano ya ligi mabingwa Ulaya baada ya kuikosa msimu uliopita walipomaliza
ligi katika nafasi ya 7.
Scholes
anamuona Di maria kama nyota atakaekuwa na msaada mkubwa katika michuano hiyo
mikubwa kwa vilabu barani Ulaya kutokana na uzoefu aliokuwa nao.
“Licha
ya yote, bado ni mchezaji bora wa fainali ya ligi ya mabingwa msimu
uliopita(akiwa Madrid), Man united wanahitaji mchezaji wa aina hii kama
wanataka kushindana katika ligi ya mabingwa, ngoja tuone ataleta nini msimu
ujao,” aliongeza Scholes.
Usajili
wa mapema wa winga wa kimataifa wa Uholanzi Memphis Memphis Depay pamoja na
uwepo wa wachezaji kama Ashley Young ambaye alikuwa na msimu mzuri Man United,
vyote vinahatarisha nafasi ya Angel Di maria katika kikosi cha kwanza cha
mashetani wekundu hao.
Tayari
tetesi kutoka katika vilabu vya Paris Saint Germain (PSG) NA Bayern Munich
kumuhitaji Muargentina huyo zimeshachukua nafasi katika vyombo vya habari kabla
ya dirisha la usajili kufunguliwa lakini awali nyota huyo alisikika akisema
angependa kuthibitisha thamani yake OLD Traffor msimu ujao baada ya msimu wa
huu kuwa mbovu kwake.
Angel Di Maria(kushoto) akiwa na mchezaji mwenzake Lionel Messi(kushoto) katika moja ya mechi za timu ya taifa ya Argentina. |
Licha ya kutofanya vizuri msimu uliomalizika ikiwa ni msimu wake wa kwanza Old Trafford, bado kocha wa timu ya taifa ya Argentina, Gerado 'Tata' Martino amemjumuisha winga huyo katika kikosi cha timu ya taifa hilo kwa ajili ya michuano ya 'Copa America'
0 comments:
Post a Comment