Thursday, May 21, 2015

Ngassa amejiunga na Free State Stars

SIKU moja tu baada ya mama mzazi wa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania aliyesajiliwa na Free State Stars ya Afrika kusini, Mrisho Ngassa, kumtaja mwanachama wa Yanga,  Shamte Mkumba kuwa ndiye aliyehusika kumzuia mwanae kujiunga na El Merreikh ya Sudan wakati huo, mdau huyo wa soka ametoa ufafanuzi wake.
Mkumba amesema yeye alimzuia Ngassa kujiunga El Merreikh kwa sababu za maslahi yake mwenyewe.
“Mrisho Khalfan Ngassa riziki yake kwenda El Merreick ilikuwa haijatimia, sahizi umeona riziki imetimia ameenda  Afrika kusini. Wananchi wajue kwamba Mrisho hakutaka kuuzwa kama gunia na ukimuuliza yeye hilo suala anajua”. Amesema Mkumba na kusisitiza: “Ngassa alitaka auzwe na apate faida, alikuwa hataki kuuzwa ili wengine wapate faida, kumbuka lile dili la El Merreikh, klabu mbili zilitaka kugawana dola laki moja na nusu za usajili, dola elfu 75 wachukue Simba dola 75 wachukue Azam. kitu kile kilimuuma sana Ngassa na hakutaka kwenda El Merreikh kwa kuwafaidisha watu wengine.

“Mrisho na Yanga wakakaa meza moja na kumpatia hela zaidi ya ile aliyotaka kwenda El Merreikh, watu wagundue hilo. Mrisho alibaki kwa faida, hakubaki Yanga kwa hasara, alipata hela zaidi ya ile ya El Merreikh, alipata mshahara mzuri na posho nzuri Yanga”.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video