Taifa Stars inaanza kutupa karata zake kesho Cosafa
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
'Makapu amecheza kwa kiwango cha juu VPL msimu huu kiasi cha kuaminika katika benchi la ufundi la Yanga linaloongozwa na Mdachi Hans van der Pluijm.'
KIUNGO wa Taifa Stars, Said Juma 'Makapu' huenda akaukosa mchezo wa kesho Jumatatu dhidi ya Swaziland katika michuano ya COSAFA utakaochezwa Uwanja wa Royal Bafokeng kutokana na maumivu ya mgongo.
Kiungo huyo chipukizi ameumia kwenye mazoezi jioni ya jana Uwanja wa Olimpia Park akijiandaa kwa mchezo huo wa Jumatatu.
Kiungo huyo amekaririwa na moja ya mitandao ya kimataifa ya michezo akieleza kuwa amejitonesha mgongo alioumia akiwa na klabu yake ya Yanga kwenye mechi za Ligi ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
Taifa Stars ipo Afrika Kusini kwa ajili ya michuano ya Kombe la COSAFA, inayoanza leo Jumapili ikiwa ni timu mwalikwa pamoja na Ghana.
0 comments:
Post a Comment