MAPEMA wiki hii gazeti la The Telegraph lilichapisha ripoti kwamba Liverpool watatumia paundi milioni 60 majira ya kiangazi mwaka huu kusajili washambuliaji watatu.
Washambuliaji hao watatu wanatakuwa Memphis Depay wa PSV , Christian Benteke wa Aston Villa na wa Burnley, Danny Ings.
Stori ya Benteke kwenda Anfield imekuwa kubwa sasa na leo gazeti la Mirror limeripoti kwamba Aston Villa wameshafanya maamuzi ya kumuachia straika huyo kwa ada ya paundi milioni 30.
Liverpool wamekuwa wakihangaika kufunga magoli msimu huu tangu kuondoka kwa Luis Suarez na inawezekana wako makini na dili la Benteke ambaye ana uwezo mkubwa wa kucheka na nyavu.
Kwa mujibu wa gazeti la Mirror, Liverpool wanataka kumuuza Raheem Sterling kwenda Man City kwa dau la paundi milioni 50 ili kutapa hela za usajili.
0 comments:
Post a Comment