HASSAN Ramadhan Kessy wa
Simba imetajwa na makocha wengi wa ligi kuu, wasiokuwa wa ligi kuu na
wachambuzi wa soka kuwa ndiye mlinzi bora zaidi wa kulia katika msimu wa ligi
kuu 2014/2015 uliomalizika mei 9 mwaka huu.
Kessy amekuwa msaada mkubwa
kwa Simba na mafanikio waliyoyapata ya kushika nafasi ya tatu yeye pia ni chachu
kubwa.
Uwezo wake wa kupandisha
mashambulizi na kugeuka kuwa winga aliyekamilika kila anapovuka mstari wa kati,
ufundi wa kupiga pasi za mwisho, kupiga krosi na kurudi kwa haraka kukaba pale
timu inapopoteza umiliki wa mpira ni miongoni mwa sababu zinazomfanya Kessy
atajwe kuwa mlinzi bora na wa kisasa wa kulia kwa sasa nchini.
Licha ya kutajwa na makocha
wengi kuwa ndiye bora, unaweza kudhani Kessy atakuwa na maneno mengi ya
kukubali sifa hizo, lakini haiko hivyo.
Kessy ameiambia MPENJA BLOG neno moja kubwa baada ya kupata
mafanikio Simba akisema: “Daah! Kiukweli Mungu ndiye anayejua kaka! Naendelea kumtumainia
na kujifunza kila siku”.
Kuhusu kutoitwa timu ya Taifa
ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ Kessy amesema: “Mpira tunacheza, kila mtu ana
malengo ya kufika mbali, lakini ndio hivyo siitwi timu ya Taifa, lakini wakati
wangu unakaribia kabisa”.
0 comments:
Post a Comment