Wednesday, May 20, 2015

LESOTHO na Tanzania ngoma droo mpaka sasa, zote zimepigwa mechi zao mbili za kwanza katika kundi B la michuano ya Cosafa inayoendelea Afrika kusini.
Swaziland wakitokea kuwachapa Taifa Stars 1-0 juzi katika mechi ya kwanza ya Cosafa, usiku huu wameichapa Lesotho magoli 2-0.
Mchezo wa mapema, Madagascar waliichapa magoli 2-0 Taifa Stars inayonolewa na kocha Mholanzi, Mart Nooij.
Kwa matokeo hayo, Lesotho na Tanzania zimetupwa nje ya mashindano hayo na zinasubiri kucheza mechi ya mwisho itakayowahusisha wao wenyewe.
Kwa timu yoyote itayoshinda mechi hiyo itapata heshima angalau ya pointi tatu, lakini haitamsaidia kitu.
Ngoma ipo kwenye mechi ya Madagascar na Swaziland.
Timu zote zimevuna pointi sita katika mechi zao mbili za kwanza.
Madagascar walianza michuano kwa kuifunga Lesotho 2-1 na leo wameichapa Tanzania 2-0.
Kwa upande wa Swaziland walianza kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania na usiku huu wameshinda 2-0 dhidi ya Lesotho.
Timu hizo zitakutana katika mechi ya mwisho kusaka mshindi mmoja atayefuzu hatua ya robo fainali ya Cosafa.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video