BONDIA Francis Cheka wa Tanzania na Kiatchai Singwancha kutoka Thailand wamepima uzito
leo kwenye ukumbi wa Green Grill uliopo maeneo ya Victoria jijini Dar es Salaam
tayari kwa pambano lao linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Masumbwi.
Pambano hilo litapigwa kesho usiku kwenye ukumbi wa PTA Manispaa ya Temeke.
Cheka
na Singwancha watazichapa kwenye pambano hilo la raundi 10 lisilo na ubingwa wowote, lakini ni mabondia hao wawili wanatafuta kulinda heshima.
Singwancha alitua Dar jana akiongozana na kocha wake tayari kwa ajili ya pigano hilo ambalo
linatarajiwa kuwa na upinzani wa hali ya juu kutokana na historia ya mabondia
wote wawili.
Pambano
hilo ambalo litakuwa ni la kwanza kwa Francis Cheka toka atoke jela
linasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa ndondi nchini ili kuona kama ataweza kumsambaratisha Mthailand huyo ambaye ana rekodi nzuri ya kupiga kwa
Technical Knockout (KO).
Cheka
amesema kuwa, anataka kuudhihirishia umma wa Tanzania kuwa bado yuko vizuri
kwenye makonde na ili kuthibtisha hilo atashinda pambano lake kesho, lakini
akawaomba wapenzi, mashabiki na wadau wa mchezo wa ngumi kujitokeza kwa wingi
kwa ajili ya kumuunga mkono ili amsambaratishe mpinzani wake.
“Jela
ni jela na ngumi ni ngumi, hakuna chochote kutoka jela kilichoathiri uwezo
wangu wa kupambana ulingoni,watanzania wajitokeze tu kuja ‘kunisapoti’ ili
nimchape mthailand. Wengi wanaujua uwezo wangu sitai kuzungumza mengi kwenye
hilo”, amesema Cheka.
“Ninauhakika
wa kushinda kwasababu mimi najua ngumi, ukiwa unajua kitu unakuwa na uhakika na
unachokifanya, kwahiyo watanzania watarajie ushindi kutoka kwangu”,aliongeza
Cheka.
Kwa
upande wake Singwancha ametamba kuwa, atashinda kwa kumpiga Cheka licha ya kukiri kutofahamu uwezo wa bondia
huyo ambaye kwa sasa anatamba kwenye masumbwi hapa Tanzania.
“Sifahamu
chochote kuhusu Francis Cheka zaidi ya kusikia jina lake, sijawahi kumuona
akiwa ulingoni. Hilo halinitishi wala kunipa wasiwasi kwasababunimejiandaa
vizuri na ninauhakika wa kushinda pambano hilo la kesho. Nimefanya mazoezi ya
kutosha chini ya kocha wangu na nipo katika hali nzuri kwa ajili ya kesho”,
Singwanchi amesema.
Takwimu
za mabondia hao
Francis
Cheka
Global
ID: 185091
Sex:
Male
Birth
date: 15 April 1982
Division:
Super middle weight
Heght
5’10.5”/ 179 cm
Current
weight: 75.7 Kg
Country:
Tanzania
Won
30 (KO 16)+Lost 8 (KO 5)+Drawn 2=40
Kiatchai
Singwancha
Global
ID: 67387
Sex:
Male
Birth
date: 17 October 1982
Stance:
Southpaw
Heght
5’ 7”/ 171cm
Current
weight: 75 Kg
Country:
Thailand
Won
35 (KO 24)+Lost 12 (KO 9)+Drawn 0=17
0 comments:
Post a Comment