KOCHA mkuu wa Simba aliyemaliza mkataba, Goran Kopunovic,
aliyepo Budapest, Hungary kwa sasa, amesema ataendelea kuwa shabiki wa Simba
kokote atakapokwenda na kusisitiza kuwa hakupenda kuondoka klabuni hapo.
“Kweli sikupenda, lakini siwezi kulazimisha. Hivyo waambie
mashabiki wa Simba nitaendelea kuwapenda sana”. Amesema Kopunovic akikaririwa
na SalehJembe na kuongeza: “Simba ilishaingia moyoni mwangu, lakini maisha ya soka
yako hivi mara zote,” alisema.
Simba imeamua kusaka kocha mwingine na sasa imetoa nafasi
kwa Mbelgiji baada ya kuonekana Kopunovic anataka dau kubwa.
0 comments:
Post a Comment