Taarifa iliyoripotiwa mchana huu na Salehjembe inasema kwamba kiungo mpya wa Yanga, Deus Kaseke
ameongezwa katika kikosi cha timu ya taifa kinachojiandaa kuivaa Misri.
Pamoja na Kaseke ambaye amejiunga Yanga kwa
dau la Sh milioni 35 akitokea Mbeya City fc, wengine watatu wameongezwa na wote
wameanza mazoezi leo kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Wengine walioongezwa katika kikosi hicho ni kipa wa Mtibwa
Sugar, Said Mohammed 'Nduda" pia beki wa timu hiyo Andrew Vincent na kiungo wa Azam FC,
Gardiel Michael.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij ambaye amekalia kuti
kavu kutokana na kikosi chake kwenda mwendo wa kusua, ameamua kuimarisha kikosi
chake na imeelezwa atafanya mchujo kabla ya kwenda Misri.
0 comments:
Post a Comment