STORI ya winga Haruna Chanongo kusajiliwa na Yanga imegonga
vichwa vya habari nchini, lakini taarifa mpya kutoka kwa Meneja wake, Jamal
Kasongo ni kwamba bado nyota huyo hajamwaga wino Jangwani.
Msimu uliopita wa ligi kuu soka Tanzania bara uliomalizika mei 9 mwaka huu, Chonongo alikuwa anaichezea Stand United ya Shinyanga.
“Ni vyombo vya habari, hatujakaa na viongozi wa Yanga zaidi
ya kunipigia simu tu!. Amefananua Kasongo na kuongeza: “Tumezungumza na kufika
mahala ambapo tumewaacha wajifikirie (Yanga) na sisi tufikirie, lakini bado
hajasaini”.
“Sijakaa mezani kuzungumza nao, nilipigiwa simu tu na
kiongozi mmoja wa Yanga na muda si mrefu nimewaambia kwamba tunapaswa kukaa
mezani”.
Kwanini Kasongo ambaye pia ni wakala wa Mbwana Samatta wa TP
Mazembe, anaweka ngumu kumruhusu Chanongo kusaini Yanga?
“Kubwa zaidi kwangu ni mkataba, kuna vipengele ambavyo nataka
lazima viwepo, unajua tunachotazama ni
hatima ya mtoto (Chanongo) kwenda mbele zaidi, nadhani kama Chanongo atakaa
zaidi ya mwaka mmoja Yanga atakuwa wa hapa hapa, nina ofa nyingi za nje,
kwahiyo nataka kujua kama Chanongo atasaini Yanga hatima yake itakuwaje?’
Amesema Kasongo.
0 comments:
Post a Comment