HATIMA ya kocha wa Simba aliyemaliza mkataba wake,
Goran Kopunovic kuendelea kuinoa klabu hiyo msimu ujao inafahamika leo ijumaa
na tayari Mserbia huyo amethibitisha kwamba leo ndio siku anakayotoa jibu
kuhusiana na ofa aliyopewa na Wekundu wa Msimbazi.
“Ni kweli
tulikubaliana Ijumaa (leo). Nitawaeleza nini kinaendelea na nimeamua vipi,’
Amesema Kopunovic na kuendelea: “Ningependa kubaki Simba, lakini kumbuka mimi
pia ni binadamu nina mahitaji muhimu,” alisema.
Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Simba,
Zacharia Hans Poppe amesema leo wanasubiri jibu la kocha huyo.
0 comments:
Post a Comment