Wednesday, May 20, 2015

TAARIFA mpya leo zinasema kocha mkuu wa Simba aliyemaliza mkataba wake, Mserbia Goran Kopunovic amekubali kurejea Dar es salaam kuendelea na kazi ya kuwanoa vijana wa Msimbazi wenye uchu wa mafanikio kuelekea msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Tayari Simba kupitia kwa mwenyekiti wa kamati ya usajili, Zacharia Hans Poppe walithibitisha kuachana na Kopunovic kwasababu ya kutaka dau kubwa la usajili na mashahara mrefu, hivyo kuanza harakati za kusaka kocha mpya.
Kopunovic alitakiwa kutoa jibu kufikia Ijumaa ya wiki iliyopita kama atasaini mkataba mpya au la!, lakini alishindwa kufanya hivyo.
Kopunovic alitaka dola za Kimarekani 50,000 (sawa na Sh. Milioni 100) kama dau la kusaini Mkataba na mshahara wa dola 8,000 (Sh. Milioni 16) kwa mwezi, kiasi ambacho Simba walisema hawawezi kulipa.
Sasa Mserbia huyo amekubali kushuka  dau na atarejea nchini kuanzia juma lijalo kusaini Mkataba mpya na mara moja kuanza maandalizi ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.

Yuke kocha Mbelgiji Piet de Mol aliyeripotiwa kuja kesho kuwania nafasi ya Kopunovic, atakuja kama kawaida, lakini kutafuta kazi klabu nyingine.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video