KOCHA wa Polokwane City, Kosta Papic ameshinda na kuwa kocha
bora wa msimu wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
Papic aliyewahi kuinoa Yanga ameshinda tuzo hiyo ya
wasomaji wa jarida la soka la Kickoff .
Kocha wa Free State Stars, Kinnah Phiri ambaye sasa anakuwa
kocha wa Mtanzania, Mrisho Ngassa naye alikuwa kati ya walioshirikishwa.
Papic raia wa Serbia amepata asilimia 38.1 baada ya kubeba
kura 787 kati ya 2066.
Phiri amepata kura 135 akiwa amezidiwa na Steve Komphela
aliyepata 370 na Rodger de Sa aliyechukua 449.
0 comments:
Post a Comment