Kocha wa timu ya taifa ya Afrika kusini ‘Bafana Bafana’, Ephraim Shakes Mashaba amesema mechi mbili za kirafiki alizocheza dhidi ya Lesotho zimemfanya agundue nini cha kufanya kuelekea juma la fainali la michuano ya Cosafa ambapo ataanza na Botswana mei 24 mwaka huu uwanja wa Moruleng.
Bafana Bafana wamecheza mechi mbili na Lesotho, mechi ya kwanza wametoa suluhu na ya pili sare ya goli moja kwa moja, huku Mashaba akikiri kuwa timu zote zilicheza soka zuri, lakini kikosi chake bado haina muunganiko mzuri.
Mechi za makundi A na B zimeanza jana ambapo mechi ya ufunguzi, Namibia imetoka suluhu dhidi ya Shelisheli na baadaye Zimbabwe ikashinda magoli mawili kwa bila dhidi ya Mauritius.
Mechi ya mapema leo ya kundi B imepigwa baina ya Lesotho na Madagascar, wakati saa 2:30 usiku kwa saa za Afrika mashariki, Taifa Stars itakuwa uwanjani kuchuana na Swaziland.
Mshindi wa kila kundi ataungana na wenyeji Afrika Kusini, Msumbiji, Zambia, Ghana, Botswana na Malawi kucheza Robo Fainali.
Kutakuwa na Nusu Fainali za aina mbili, kwanza ya timu zilizofungwa katika Robo Fainali (Plate Semi Finas) na zilizoshinda (Semis Finals).
Vibonde wataendelea kupepetana hadi fainali yao ambayo itapigwa Mei 29, wakati fainali ya wakali itakuwa Mei 30.

0 comments:
Post a Comment