Friday, May 1, 2015

KIUNGO mkongwe wa Mbeya City fc, Steven Mazanda 'Babu' amewashukuru wachezaji wenzake kufanya kazi nzuri wakati huu yupo nje ya uwanja kutokana na majeraha ya misuli yanayomsumbua.
Mazanda aliyeumia kwenye mechi dhidi ya Ruvu Shooting februari 28 mwaka huu amekosa mechi nane (8) za Mbeya City mpaka sasa na tayari timu hiyo imebakiza mechi mbili tu dhidi ya Prisons jumamosi hii na mei 9 mwaka huu itachuana na Polisi Morogoro, mechi zote zinachezwa uwanja wa Sokoine.
Mbeya City kwa sasa wanashika nafasi ya nne wakiwa na pointi 31 baada ya kucheza mechi 24 sawa na Kagera Sugar wanaoshika nafasi ya tano kwa pointi 31, lakini City wana wastani mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa.
City wameshinda mechi 7, wamefungwa mechi 7 na sare 10, Wamefunga magoli 21 na kufungwa 21, tofauti ni 0, wakati Kagera Sugar wameshinda mechi 8, wamefungwa mechi 9 na sare 7, wamefunga magoli 22 na kufungwa 24, tofauti ni -2.

Mazanda ameiambia MPENJA BLOG: "Hali yangu iko poa, nashukuru wadogo zangu wanafanya kazi nzuri, acha wamalizie mechi hizi zilizobaki na hata viongozi wanalijua hilo. Naendelea vizuri, lakini sio kwamba naweza kucheza, ujue kazi ya mpira sio rahisi, inahitaji nguvu ya mwili, acha nikae sawa kabisa mpaka msimu ujao"
"Niliumia misuli, ni muda hata wewe mwenyewe unaweza kushangaa, ilikuwa mechi na Ruvu Shooting hapa Mbeya, niliumia kama dakika ya 70, lakini nilimaliza mechi na hakuna mtu aliyekuwa anajua, niliumia sana siku hiyo".

ANATOA USHAURI GANI KWA VIJANA WA MBEYA CITY FC?

'Babu' Mazanda anasema: "Nawashauri vijana, mpira ni kazi yao, pamoja na changamoto tuliyokutana nayo msimu huu tunatakiwa kuangalia mbele tu na kuweza kurudisha heshima yetu iliyoshuka. Safari ya mpira ni ndefu kidogo hata mashabiki waelewe kuwa inahitaji uvumilivu".

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video