Katika mazoezi ya jana usiku kocha mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amewaambia vijana wake kujiamini na kucheza soka la kushambulia ili kufunga magoli ya mapema na kuwachanganya Etoile du Sahel katika mechi ya kesho usiku kuanzia majira ya saa 3:00 usiku kwa saa za Tanzania.
Mkuu wa Idara ya habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro naye kama kawaida yupo Tunisia kufuatilia mambo yanavyokwenda. Yanga wanahitaji ushindi au sare ya angalau magoli 2-2 ili kusonga mbele moja kwa moja kwasababu mechi ya kwanza jijini Dar es salaam timu hizi zilitoka sare ya 1-1
Maelekezo ya hapa na pale kabla ya kuanza mazoezi
Mrisho Ngassa (kushoto) na Simon Msuva (kulia) wanatarajia kuongoza safu ya ushambuliaji leo
0 comments:
Post a Comment