Wednesday, May 20, 2015

MLINDA Mlango mahiri wa Mbeya City Fc Haningtony Kalyesubula amesema amefurahishwa  na matokeo  aliyoyapata msimu huu kwenye kikosi cha klabu hiyo.
Akizungumza na mapema leo muda mfupi kabla ya kupanda ndege kurudi nyumbani kwake nchini  Uganda kwa mapumziko ya mwisho wa msimu,  Haningtony amesema kuwa awali wakati anajiunga na City hakujua kama timu hii imejipanga vizuri pengine kuliko zote alizowahi kupita.
“Nimefurahishwa na mambo jinsi yanavyoendeshwa hapa, ndani ya uwanja timu ina mashabiki wengi na wenye nguvu na moyo kwa timu yao, hakika jambo hili liliniongezea nguvu ya kuwajibika uwanjani, maslahi ni mazuri pia katika hili siwezi kuficha ukweli kuwa nimekuwa na msimu mzuri sana kwenye kikosi cha City”alisema Haningtony.
Golikipa huyu mahiri alijunga na City mwanzoni mwa msimu uliomalikazika lakini alishindwa kujumuishwa kikosini mapema kufuatia kuchelewa kuwasili kwa hati yake ya uhamisho kutoka shirikisho la Uganda FUFA. 
Amecheza michezo 9 na ameruhusu mabao 8 huku pia akifanikiwa kuzuia michomo 12 ambayo dhahiri ilikuwa mabao ya wazi kwa timu pinzani.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video