MCHEZAJI wa timu ya taifa ya Tanzania chini ya miaka 20, Hija Mohamed Ugando leo anaanza majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Atalanta Bergamo ya Italia ili kujiunga na timu B.
Nyota huyo aliyekulia kwa miaka yote 'JAKI Football Academy' ya Mbagala na kucheza ligi daraja la pili akiwa na Mbagala United aliondoka siku tatu zilizopita akitokea nchini Tunisia alipokuwa anafanya majaribio katika klabu kubwa ya CS Sfaxien.
Wakala wa mchezaji huyo ambaye pia ni wakala wa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayecheza TP Mazembe ya DR Congo, Jamal Kisongo ameueleza mtandao huu kuwa Ugando anaanza majaribio yake leo.
Pia ameeleza kwa kifupi wasifu wa kinda huyo;
"kwa miaka yote amekulia JAKI Football Academy ya Mbagala na alicheza ligi daraja la pili na Mbagala United. Baada ya hapo tulimtoa kwa mkopo kwenda Nakuru Top Fly inayocheza ligi kuu Kenya, baadaye akarejea hapa (Tanzania) na tukampleka CS Sfaxien ya Tunisia kufanya majaribio". Ameeleza Kisongo na kuongeza: "Yule wakala wetu alikuwa hajamuona, tulizungumza tu kwa mdomo, kwa bahati nzuri akamuona mwenyewe kwa macho yake akiwa Sfaxien, akaghaili kuwa huyu si mchezaji wa Afrika, huyu ni mchezaji wa ulaya, kwahiyo akamtafutia nafasi Atalanta na sasa yuko huo. Pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20, majaribio yake anaanza leo".
0 comments:
Post a Comment