MABINGWA wapya wa soka Nchini Tanzania,Young Africans leo wanateremka dimbani Kwenye uwanja wa Anex Olympic de Sousee nchini Tunisia kupambana na Etoile du Sahel katika mchezo wa marudiano unaotarajiwa kuchezewa usiku Majira ya 3:00 kwa saa za Afrika mashariki.
Yanga ambayo tangu iwasili nchini Tunisia mbali na kukumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya kimazingira na haswa hali ya hewa ya mji wa Sousee kuwa ya baridi Sana nyakati za usiku,wachezaji wakiongozwa na Mwalimu Mkuu wa Timu Mdachi Hans van Pluijm akisaidiwa na Charles Boniface Mkwasa wamefanya mazoezi yao Ya mwisho katika uwanja wa Anex Olympic de soussee ambao ndio utakaotumiwa leo katika mchezo wao dhidi ya Etoile.
Kwa upande wake Mkuu wa idara Ya Habari na Mawasiliano wa Yanga , Jerry Cornel Muro amesema wao Kama uongozi wameiandaa timu Kwa kuhakikisha wanatengeneza mazingira bora Ya Kambi na kuhakikisha wanadhibiti vitendo vyote vya hujuma nje na ndani Ya uwanja na Kuwataka Watanzania kuendelee kuiombea timu yao ili waweze kufanya Vizuri.
Katika kuhakikisha Yanga inaibuka na ushindi,baadhi ya Wachezaji wa Yanga wamewaahidi watanzania ushindi Kwa kupambana kufa na kupona huku kiungo aliyekuwa majeruhi Kwa muda, Salum Telela akiwa anerejea Uwanjani katika ubora wake .
Kwa upande wao baadhi Ya mashabiki,wanachama na wapenzi wa Yanga walioambatana na timu hiyo nchini Tunisia wamesema Kwa mazoezi waliyofanya Yanga timu ina kila Sababu Ya kuibuka na ushindi katika mchezo wa leo.
0 comments:
Post a Comment