Thursday, May 21, 2015

Mandawa (kulia) akijaribu kumpiga chenga mlinzi wa Yanga, Rajabu Zahir walipochuana uwanja wa Taifa msimu uliopita. Kagera Sugar ilifungwa 2-1.

MTANDAO huu jana uliripoti taarifa za Straika hatari wa Kagera Sugar, Rashid Mandawa kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia timu ya Mwadui fc iliyopanda kucheza ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2015/2016.
Leo hii tunakuletea kauli aliyosema Mandawa baada ya kuanguka kandarasi hiyo kuwatumikia matajiri hao wa Madini wanaotarajiwa kusumbua katika soka la Bongo.
“Kikubwa ni kumuomba mwenyezi Mungu, yeye ndiye mpangaji wa kila kitu, yeye ndiye alinitoa kutoka chini na kuwa moja ya wafungaji bora. Namuomba Mungu anizidishie zaidi ya hapa ili msimu ujao niweze kuchukua kiatu cha ufungaji bora”, Amesema Mandawa na kusisitiza: “Mimi msimamo wangu kama tulivyosaini mkataba , nitasaini mkataba mwingine pale utakapoisha, siwezi kusaini mkataba wakati nina mkataba mwingine, kwanza nitakuwa najihatarisha mimi mwenyewe na uchezaji wangu, unaweza kufungiwa miaka miwili na mimi kazi yangu mpira.

Mandawa alifanikiwa kufunga magoli 10 akiwa na Kagera Sugar msimu wa 2014/2015 uliomalizika mei 9 mwaka huu.
Simon Msuva wa Yanga ndiye aliyeibuka mfungaji bora wa ligi kuu baada ya kutikisa nyavu mara 14.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video