Saturday, May 23, 2015

Sami Khedira ametoa shutuma nzito dhidii ya timu yake ya Real Madrid kwa kumlazimisha kuondoka, huku akisisitiza kuwa kocha wa klabu hiyo Carlo Ancelotti alielekezwa kutokumpanga.
Kiungo huyo raia wa Ujerumani anatarajia kuondoka klabuni hapo mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu, msimu huu Khedira amefanikiwa kuanza katika michezo 7 tu.
Tatizo kubwa ambalo limekuwa likimsumbua Khedira ni majeraha ya mara kwa mara, lakini kwa uapnde wake amesema hiyo sio sababu kubwa iliyomfanya awekwe benchi. Kherdira kwa sasa ana umri wa miaka 28.
"Siku zote unapaswa kuongea ukweli. Nilikuwa nikisumbuliwa na jeraha dogo tu, maumivu katika kisigino changu cha kulia, lakini hiyo haikuwa sababu ya mimi kutocheza. Halikuwa jeraha kubwa sana, nilikuwa na uwezo wa kucheza," Khedira aliliambia gazeti la Marca.
"Siku zote nimekuwa nikiamini nina sapoti kutoka kwa kocha, lakini ujumbe ambao ulikuwa si wa moja kwa moja ulinifikia ukisema nilikuwa sihitajiki tena klabuni hapo, nilishatupwa nje na nisingekuwa na nafasi tena ya kuendelea kucheza klabuni hapo.
"Hakuna yeyote hapa klabuni aliyenifuata na kuniambia chochote kile. hapo hisia, nikichanganya na matukio yaliyopo nikaanza kuamini kuwa siwezi kucheza tena. Maana hakuna yeyote aliyenifuata.
"Kulikuwa na vikao vingi sana. Cha mwisho kilikuwa ni mwezi Oktoba. Baada ya mjadala marefu, sikuwa na uhakika kama ningepewa mkataba mpya wa miaka minne. Nilikuwa na wasiwasi na ndipo mwezi Disemba niliona ni bora nitafute njia nyingine ili kupata changamoto mpya kuliko kuendelea kubaki hapa."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video