Wanachama wa timu ya soka ya Toto Africans ya Mwanza kesho
tarehe tatu mwezi tano wanatarajia kufanya mkutano wao mkuu jijini humo.
Mkutano huo ambao umeitishwa na wanachama ambao walikusanya
saini hili kuushinikiza uongozi wa timu hiyo kuitisha mkutano wao kama
katiba ya timu inavyotaka.
Kwa mujibu wa katiba ya timu hiyo mkutano wa timu hiyo
ulipaswa kufanyika toka mwishoni mwa mwezi wa tatu ama mwanzoni mwa
mwezi wa nne lakini ukashindwa kufanyika.
Akizungumza na Mpenja
blog,makamu mwenyekiti wa timu hiyo Ahmed Waziri Gao amesema kuwa
mkutano ni haki ya wanachama ambao ndio wenye timu kwa hiyo uongozi
hauna pingamizi kama taratibu zimefuatwa.
"Katiba yetu inatutaka tuwe na mkutano mkuu na sio timu
yetu ni timu zote zinafanya hivyo kwahiyo wanachama wametumia haki yao
ya msingi hivyo mkutano wetu utafanyika tarehe tatu mwezi huu pale shule
ya msingi Nyamagana"Alisema Gao.
Aliongeza kuwa katiba ya timu inasema baada ya wanachama kuomba mkutano,mkutano utaitishwa baada ya ya wiki mbili.
"Katiba inasema hivyo wala si Mimi Gao kwamba baada ya kuomba mkutano,mkutano utafanyika baada ya wiki mbili na hilo liko wazi"
Kadhalika makamu mwenyekiti amezitaja baadhi ya agenda kuwa
ni kujaza nafasi zilizoachwa wazi na mwenyekiti bwana Omary Mbalamwezi
na wajumbe wa kamati ya utendaji ambao ni Gasper Mwanalelya na Godfrey
Kyabula ambao wote walijiuzuru kwa nyakati tofauti.
"Hatutakuwa na uchaguzi kwenye mkutano huo ila tutakuwa
tunajaza nafasi ambazo ziko wazi baada ya wenzetu wale kujiuzuru
,kwahiyo hakutakuwa na uchaguzi mpaka pale katiba yetu itakapofanyiwa
marekebisho".Alifafanua
Kwa upande wa mwanachama ambaye alikuwa anakusanya sahihi hizo kutoka kwa wanachama wenzake aliyejitambulisha kwa jina la Salehe,Ameupongeza uongozi na kusema kuwa wao kama wanachama lengo lao ni zuri juu ya timu yao.
Kwa upande wa mwanachama ambaye alikuwa anakusanya sahihi hizo kutoka kwa wanachama wenzake aliyejitambulisha kwa jina la Salehe,Ameupongeza uongozi na kusema kuwa wao kama wanachama lengo lao ni zuri juu ya timu yao.
"Kama unavyojua timu yetu itashiriki ligi msimu ujao
kwahiyo tunahitaji kupanga jinsi ya ushiriki wetu,kuna wajumbe na
mwenyekiti wamejiondoa kwenye timu lazima tujaze nafasi zao timu haiwezi
kuongozwa na wajumbe watatu tu na la mwisho tumeshiriki ligi daraja la
kwanza mpaka tumepanda ligi kuu timu ilikuwa inatumia pia kupata pesa
tunahitaji kupewa ufafanuzi wa vitu kama hivyo".Alizungumza Salehe.
0 comments:
Post a Comment