HII ndio kauli ya kocha mkuu wa Prisons, Mbwana Makata
kuelekea mechi ya kesho dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Sokoine, Mbeya.
“Hatuna namna ya kuepuka kushuka daraja zaidi ya kushinda
michezo miwili iliyobaki kuanzia wa kesho na Mbeya City. Najua itakuwa mechi
ngumu, lakini tutapambana kwa nguvu zetu zote. Nimewajenga wachezaji
kisaikolojia, nashukuru sasa hivi wachezaji wanaimarika sana, wanajituma kwa
hali ya juu”.
Prisons wapo nafasi ya 12 wakijikusanyia pointi 25 sawa na
Ndanda fc wanaoshika nafasi ya mwisho, lakini Wajelajela wana wastani mzuri wa
magoli ya kufunga na kufungwa.
Ndanda wamefunga magoli 18 na kufungwa 29, tofauti ni -11,
wakati Prisons wamefunga magoli 17 na kufungwa 22, tofauti ni -5.
0 comments:
Post a Comment